PETE MBILI KIDOLENI Sinja xxxx xxx@gmail.com BOX 568-xxxxxx TURBO 0721561xxx Wahusika Waliomo Mchezoni CHIPOLOPO Kijana.Rafikiye Nina na Kanta. BAKORA Mzee.Babao Kanta,Nina,Tibato na Tabita. NINA Dadao Kanta,Tibato na Tabita. KANTA Kakao Nina,Tibato na Tabita. TABITA Dadao Kanta,Nina na Tibato. TIBATO Kakao Kanta,Nina na Tabita. SANMA Mkewe Bakora.Mamao Kanta,Nina,Tibato na Tabita. DANMA Shangazi wao Kanta,Nina,Tibato na Tabita. NISI ‘Mkewe’ Kanta. ONYESHO LA KWANZA. SANMA:(Anachomoza kichwa dirishani,na kutazama nje kisha anaurudisha ndani.) Mvuke leo,unasambaa isivyotarajiwa. Kulikoni,au kunaungua mahali? (Anapiga miluzi,kisha anaacha tena.) Sio kama zama zetu,ambapo majira yalikuwa mahususi. Au,inaonekana mvua itanyesha mapema leo.Hata hivyo,ndivyo tu jinsi mambo huwa wasa unapopita.Mvuke huu sio wa kawaida. (Anamgeukia Nina) Nina! NINA:Mama. SANMA:Kachukue vyombo hivi,ukavisafishie kule nje. NANA:Ndio Mama.(Anachukua sahani kadha,sufuria miongoni mwa vyombo vingine,kisha anatokomea nje.) TABITA:Mama usiku wa leo sikulala vyema. SANMA:Macho yalidinda kufumba ama! TABITA:La! Tibato alishinda akiivuta blanketi kuelekea upande wake. TIBATO:Uongo. TABITA:Ukweli.Sehemu kubwa ya blanketi iliishia kwako. TIBATO: Blanketi yenyewe si blanketi.Imejaa matundu hata nyota angani zahesabika. TABITA:Mama umemsikiza. NINA:(Anaangua kicheko,nje alipo.) Lo! Ulimwengu hauishi mambo.Watoto hawa,viroja tupu.(Anachukua mojawapo ya sahani na kukiosha majini kwa vidole vyake.Uchafu unadinda kuondoka.) Aha! (Anachukua sabuni na kupakia kwenye msuguo.Kisha anaiosha sahani yenyewe tena.Uchafu pamoja na rangi iliochorewa ua kwenya sahani inaondoka.)Mbona!Kumbe ndio sababu mzee amekuwa akilalama kuhusu maumivu tumboni. SANMA:Ninyi na huo ugomvi-sarakasi yenu mtatokomea kule! (Kwa Tibato) Kawafungulie kuku.Sio vyema niwe nikikukumbusha siku nenda… TABITA: Siku rudi. SANMA: (Kwa Tabita kwa hasira..)Funga domo.Sijaulizia usaidizi wako.Tafuta ufagio,ukaondoe uchafu wote upenuni.Hata unyasi usionekane.(Bado wamesimama huku wamemkodolea macho.) Sasa hivi. (Wanafanya kuondoka) TABITA:Wewe umeula muwa wangu na kuubadilisha na bingobingo. TIBATO:Ati nini? TABITA:(Akiugusagusa tumbo lake Tibato kwa bingobingo.)Ndio,muwa wangu uko wapi? SANMA:Nendeni kwa shughuli nilizowatuma haraka.(Anaingia Nina.) Ni vyema umeingia.Tafadhali keti,tupige gumzo kidogo.(Nina anavuta kiti kidogo kilichochoka hivi karibu naye,kisha anaketi juu yake.Kiti kinatoa sauti ya lalama,ambazo bila shaka ungekubali ni ya maumivu na maonevu.)Binti wangu,nisikilize… TIBATO:(Kwa Tabita,wakiondoka.) Uliuweka wapi? TABITA:Muwa wangu ninautaka sasa hivi la sivyo uionje hamaki yake baba. TIBATO:Muwa wenyewew hata siujui.Sina fununu ulivyokuwa ukifanana. TABITA:Twende. (Akimvuta shati.) Tutayatatulia mbele,kwa baba.(Wanamkaribia Mzee Bakora ambaye anapunga hewa iliyosheheni,mvuke upenuni,huku akikipapasa kijibwa chake.) Baba ! Baba! BAKORA:Nini nanyi kunijia hivo kwa kisirani mapema hivi! TABITA:(Akimwashiria Tibato) Ameula muwa… BAKORA:Twende.Tutayashughulikia ndani. (Wanaingia ndani ya msonge wa pili.Mzee bakora anazama kitini huku Tabita na Tibato wakiketi mkekani.) Masahibu yenu yapi? TABITA:Ameula muwa wangu,halafu akaubadili na… TIBATO:(Anamkatiza) Sijabadili na chocho… BAKORA:Nyamaza! TIBATO:Akaubadilisha na bingobingo. BAKORA:Tibato,kumbe wewe mkorofi hivi! TIBATO:Hapana Baba. BAKORA:Mbona hivi? TIBATO:Hivi aje baba! BAKORA:‘Hivi aje baba’.Mbona kumtenda (Akimchuna masikio yote mawili.) dadako hivi? (Nje mlangoni Kanta na Nisi wamekwisha wasili kutika mjini.Wanaangua kicheko.) TIBATO:Baba tafadhali. BAKORA:Afadhali nini? TIBATO:Nisikize tu,hata ikiwa tu,ni kwa sekunde moja.Tafadhali. BAKORA:Jitetee TIBATO:(Kwa Tabita) Sema ukweli,tangu jadi hadi leo,ipo siku nimewahi kukichukua au kukila chochote chako? TABITA:Hapana. TIBATO:(Kwa Mzee Bakora) Baba Kesi imetamatika. (Kwa furaha.) Amekiri mwenyewe kuwa sijawahi kugusa chochote chake. TABITA:Hapana,hiyo sio haki. TIBATO:Baba,si hata wewe ulimsikiza vyema. (Kanta na Nisi wanacheka tena) KANTA:(Kwa Nisi wakiingia) Toto hili la mama haliishi mizungu. BAKORA:(Wakiamkuana) Karibu sana bakora yangu,karibu. KANTA:Asante baba. BAKORA:Karibu.Ninaona kidogo (Akimpekua Nisi) una mwenzako. NISI:(Kwa tabasamu ya hamnazo) Tunashukuru. KANTA:Huyu ndiye…(Wanaendelea na mazungumzo yao kwa kiasi.) NISI:(Kwa Tibato) Upanda uvutiao shingoni mwako ninauona. TIBATO:(Akitabasamu) Ni mzuri sana. NISI:Kakutengenezea nani? TIBATO:Mie mwenyewe,madhumuni yakiwa ni kuwapiga tu mwewe wanyemeleapo vifaranga vyetu. NISI:Hewalla! TIBATO:Asante.Ndivo ilivyo. NISI:Na,hufanya kazi vipi? TIBATO:Hivi.(Anautumbukiza mkonowe mfukoni na kuchomoa jiwe moja dogo.Anauweka sawasawa katika panda na kumlenga shabaha mbwa wake Mzee Bakora,aliyeketi karibu naye.Mbwa anatokomea nje,huku atoa kilio cha maumivu makali.) BAKORA:(Kwa ghadhabu) Wampigia nini mbwa?Kakukosea nini mbwa wangu? (Wote waliopo wanaangua vicheko.) KANTA:(Akiokota jiwe lenyewe sakafuni.) Hebu,(Kwa Tibato.) Hebu.(Tibato anamkabidhi panda.)Kifaa hiki kidogo. (Kama Tibato hapo awali,analiweka jiwe sawasawa katika panda.Pasipo na ufahamu wa jinsi ya kuitumia,anajilenga shabaha puani.Wote waliopo wanaangua vicheko.) BAKORA:(Akipiga chafya.) Uvundo mbovu huu,nao unatokea wapi? (Anapiga tena.) Nani kaharibu hewa hapa? (Akimgeukia Tibato) Ni wewe. TIBATO:Hapana Baba.(Waliopo wanacheka.) BAKORA:Songa mbali.Ni nani kama sio wewe? TIBATO:Mie sijui.Niamini baba,mimi sie. (Wanaingia Sanma na Nina.) SANMA:(Akimkumbatia Kanta,halafu Nisi.) Karibu sana mwanangu. KANTA:Asante mama.(Wanaamkuana pia na Nina. ) Tumesikia mazungumzo yaliyo sheheni furaha,ikiwemo vicheko.Tukanga’amua ah,lazima mmeingia.Ya mjini? KANTA:Kwema mama. SANMA:Wajukuu wangu ..vipi? NISI:Hawajambo mama. SANMA:Ninafurahi kusikia hilo. KANTA:Asante mama.Nimekuja kuwajulieni hali,na pia kuahidi kumchukua,(Anamshika mzee Bakora bega ambaye anaitikia kwa kutikisa kichwa.) mzee wangu huyu,aghalabu aje awe na ufahamu wa aishiko mwanawe. SANMA:Ni vyema mwanangu. NINA:(Akipiga chafya.)Leo nayo,kiwanda kimetoa uchafu Zaidi.Kijana aliyeleta maziwa asubuhi alisema kuwa mto ulikuwa na maji ya rangi.Samaki walionekana wakielea juu majini.(Wote waliopo wanaangaliana kwa mshangao.) Hata hewa imechafuliwa na moshi unaotoa uvundo mbaya hivo. (Kila mmoja anamaka.) KANTA:(Kwa Bakora.) Baba,afya vipi? Matatizo yale ya figo na tumbo bado yanatatiza? SANMA:(Akimnong’onezea Nina.) Njoo.Twende tukapange jinsi tutaandika meza. (Anaitikia Nina,kisha wanaondoka.) BAKORA:Imeimarika kwa kiasi kikubwa,pindi nilipoacha kutumia vile vitu,sijui vya mapakiti na bidhaa zilizopakiwa. KANTA:Kweli? BAKORA:Bila shaka.Na pia niliporudia sahani zangu za udongo na na za buyu.Maumivu yamepungua,yapata mwezi sasa. TABITA:(Kanta kwa furaha anamkumbatia Mzee wake.Tibato na Tabita wanajiunga pia.) Unaelekea kupata nafuu baba. BAKORA:Natumai. KANTA:Ulikuwa unakupa kiwewe,nasi pia. BAKORA:Maumivu hayo yalikuwa yananizidi. (Nisi anabaki amewatazama mzee na wanawe wakiwa wamekumbatiana kwa furaha.Anafurahia pia.Anapiga makofi.Msonge unajawa na joto la furaha.)